Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:40 am

NEWS: WAZIRI MKUU MAJALIWA ASEMA CHANGAMOTO ZA AJIRA NCHINI ZAPUNGUA

Dar es Salaam: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tatizo la vijana kukosa ajira l imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.

Majaliwa aliyasema hayo jana Oktoba 6, 2018 alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha Bukop na kile cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na kitengo cha mawasiliano cha ofisi ya Waziri Mkuu kimemnukuu Majaliwa akisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Image result for kassim majaliwa

Alisema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa.

Waziri Mkuu alisema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800.

“Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne iliyoanza jana, inayolenga kufuatilia maendeleo ya viwanda na zao la kahawa, ambalo ni kati ya mazao makuu sita ya biashara.

Image result for viwanda tanzania

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Bernad Limbe kuhakikisha anatafuta eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo.

Aliyasema hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika eneo la bandari na kuondolewa bila ya kupewa eneo lingine.

Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya kufanyia biashara bila kuwaonyesha eneo lingine ambalo watalitumia kwa aliji ya kufanyia biashara zao.

Awali, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Linus Leopord alisema kwa mwaka wanazalisha tani 600 za kahawa iliyokaangwa na kusagwa, ambayo inatosheleza kwa mahitaji ya soko.

Pia, kiwanda cha kahawa cha Tanica kina uwezo wa kuzalisha kahawa ya unga tani 500 kwa mwaka ila kutokana na uchakavu wa miundombinu kinazalisha tani 300 kwa mwaka.

Kuhusu masoko Leopord alisema kwa sasa mauzo yameongezeka, wanauza tani 50 ya kahawa iliyokaangwa na kusagwa kwa mwezi, ambapo awali walikuwa wanauza tani 32.

Meneja huyo alisema wameimarisha na kuongeza soko la nje ambapo kwa sasa wanauza tani 35 za kahawa ya unga kwa mwezi, awali walikuwa wanauza tani 20.

Alisema kiwanda cha Tanika kinamilikiwa na Chama cha Ushirika cha KCU (53.37 %), KDCU (31.8%), Hazina (7.67), TFC (6.22%) na wafanyakazi wa Tanica (0.92%).


Chanzo: MCL Digital