- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU AWAONYA MAAFISA ELIMU KWA WIZI WA MITIHANI
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaonya maafisa elimu na walimu kutojihusisha na vitendo vya wizi wa mitihani vinavyofanywa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kwa sababu vinawadharirisha.
“Kama kweli umemuandaa mtoto huna sababu ya kuiba mitihani na mtoto hawezi kufikiria kuiba mitihani kwa sababu yuko nje ya mfumo. Walimu heshimuni maadili ya kazi ya ualimu.”
Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumanne, Oktoba 9, 2018) baada ya kukabidhiwa vyumba vya madarasa vya shule za msingi Nyakato na Kashozi, wilayani Bukoba.
Vyumba hivyo vilivyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japan baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka 2016.
Waziri Mkuu amesema tathmini ya elimu katika shule za msingi na sekondari hufanyika kwa kufanya mitihani, dosari ya udanganyifu wa mitihani iliyojitokeza katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu isijirudie tena.
Wiki iliyopitaBaraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilifuta matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa shule za msingi zote za Halmashauri ya Chemba na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuvujisha mitihani.