- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU ATAKA UCHUGUZI WALIOTAFUNA MIL 700
LINDI: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuunda Jopo la wataalamu kuzifuatilia Sh milioni 700 zilizotolewa na Serikali kukarabati Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea ambazo hadi sasa hazijatumika hata kidogo.
Pia Mh Majaliwa ameitaka timu hiyo kukagua matumizi ya Sh milioni 400 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi Kituo cha Afya cha Kata ya Kilimarondo ambazo zimeisha kabla ujenzi haujakamilika.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana Jumamosi, Novemba 17, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kilimarondo, Nachingwea mkoani Lindi, baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya
“Serikali haitaki mzaha na fedha za umma, hivyo Mkuu wa Mkoa unda timu ya wataalamu kutoka mkoani waje Nachingwea kufuatilia ni kwa nini fedha zimetolewa tangu Julai ili kukarabati hospitali ya wilaya ziwe hazijatumika hadi leo. Pia tujue kama kweli bado zipo,” amesema.