- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU ASHTUKIA UBADHIRIFU UJENZI HOSPITALI YA SONGEA
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na gharama kubwa zilizotumika katika ukarabati wa jengo la kupumzikia akina mama wajawazito lililojengwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa mjini Songea ambalo limegharimu shilingi milioni 129 huku akimuagiza Naibu Waziri wa afya, Dkt. Faustine Ndungulile kufuatilia gharama hizo na kuwachukulia hatua wote waliohusika kuhujumu fedha za serikali.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati akikagua jengo hilo katika hospitali ya rufaa ya mkoa mjini Songea pamoja na kuetembelea wodi ya watoto kabla hajazindua mashine ya kisasa ya kidigitali ya X-ray katika hospitali hiyo kwa niaba ya hospitali zingine nne za geita, mwanza, simiyu pamoja na Morogoro.