Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:46 am

NEWS: WAZIRI MKUU AITAKA TANESCO KUHAKIKISHA UPATIKANAJI WA UMEME HARAKA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Meneja wa TANESCO wilaya ya Ruangwa, Bw. Samuel Pyuza kuhakikisha umeme unapatikana mapema kwenye pampu ya maji ili kukamilisha mradi wa maji wa Namahema ‘A’.

Akizungumza na wakazi wa vijiji vya Namahema ‘A’ na Namahema ‘B’ wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kukagua mradi wa maji ambao unatarajiwa kukamilika Januari 15, mwakani.

''Mradi huo utagharimu Sh. milioni 244.52, na utahudumia wakazi 2,257 wa vijiji hivyo viwili ambao walikuwa wanasongamana kupata maji kutoka kwenye kisima ambacho kilikuwa kinatumia pampu ya mkono''. Alisema Majaliwa

Waziri Mkuu yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, lakini ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Jumla ya sh. milioni 189.93 zimeshatumika kwenye mradi huo ambazo ni sawa na asilimia 77.68 ya fedha ziliopangwa kutumika. Kijiji cha Namahema ‘A’ kina watu 1,668 na Namahema ‘B’ kina watu 589