- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA UTENDAJI WA PROGRAMU YA MIVARF.
DOM: Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameridhishwa na Utendaji wa Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kuendelea kuwafikia wananchi walioko vijijini katika kupanua huduma za kifedha na miundombinu ya masoko .
Ametoa pongezi hizo hii jana (Oktoba 3, 2018) alipokutana na Watendaji wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Kujadili Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 na Maagizo 19 ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli aliyoyatoa wakati wa kikao chake cha Novemba 20, 2015 alipokuwa akifungua kikao cha kumi na moja cha Bunge Jijini Dodoma.
“Mradi wa MIVARF umekuwa na tija kubwa kwa jamii hususan katika kukuza uchumi na maendeleo kwa Watanzania hasa katika kuendelea kupanua huduma za fedha hadi vijijini, uwezeshaji wakulima na asasi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo ya pembejeo za Kilimo pamoja na ujenzi wa miundombinu ya masoko na maghala bora ya kuhifadhia mazao hasa vijijini.”Alisema Waziri Mhagama.
Aliongezea kuwa, Program ya MIVARF imekuwa ya mfano kwa kuzingatia utekelezaji wake hapa nchini kwa kuendelea kuwaunganisha wakulima na Asasi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo ya pembejeo , zana bora na mashine ambapo tayari huduma za kifedha zimepanuliwa na kufikia watu zaidi ya milioni 4 nchini, wakulima wadogo wapatao 83,988 waliounganishwa kupata mikopo ya mbolea, mbegu, pembejeo, mashine ndogo na zana bora za usindikaji mazao kwa kupitia vikundi vyao kuongeza chachu ya ukuaji wa uchumi nchini.
Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira, na Vijana Mhe.Anthony Mavunde aliunga mkono pongezi za Waziri kwa kueleza jitihada zinazofanywa na Programu hiyo ya ujenzi wa masoko Bara na Visiwani na hivyo kuendelea kuimarisha Muungano kati yao.
“Binafsi ninawapongeza sana watendaji wote wa MIVARF kwa kazi kubwa mnayoifanya hususan kutekeleza programu hii hadi Visiwani na kuleta chachu ya mahusisno mazuri yanayoimarisha Muungano wetu.”Alisisitiza Mavunde.
Kwa upande wake Mratibu Taifa wa Programu hiyo Bw.Walter Swai alieleza mafanikio ya programu hiyo wakati wa uwasilishaji wa mada yake kuwa, Programu imeweza kunufaisha wananchi 10,019 kutokana na uhifadhi wa mazao yao katika maghala 29 yaliyojengwa na amasoko 14 hivyo kuwezesha wakulima kuhifadhi tani 16,810 ikiwa ni pamoja na uwezeshwaji wa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 420.4.
Aliongezea kuwa, tayari programu imewezesha jumla ya vikundi 37 kupata mashine za kusindika mazao ili kuongeza thamani na kuongeza ajira nchini.
AWALI
Programu ya MIVARF inafanya kazi na Taasisi/Asasi mbali mbali za kifedha.Taasisi hizi ni pamoja na Wizara ya Fedha na Benki Kuu katika kuboresha sera na sheria za utoaji wa huduma ndogo za kifedha nchini, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar pamoja na Chuo Kikuu cha Ushirika; ili kuimarisha utoaji wa huduma katika vyama vya ushirika nchini, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kuweka utaratibu unaoboresha utoaji wa huduma za kifedha kupitia mifumo isiyo rasmi, ili kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha vijijini. Mradi ulianza kutekelezwa mnamo Mwaka 2011 na unatarajiwa kuisha Machi 2019.