- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MHAGAMA AFUNGA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI MKOANI ARUSHA
ARUSHA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) amezitaka halmashauri kutambua mahitaji ya sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuleta mabadiliko chanya na maendeleo kwa sekta hizo nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri huyo wakati akifunga maonesho ya wakulima na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini Mkoani Arusha. Maonesho hayo yanafanyika katika uwanja wa Themi Njiro yakiwa na Kauli Mbiu: Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.
Alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano imeendelea kuonesha adhima ya dhati katika kuhakikisha wakulima, wafugaji na wavuvi wananufaika nchini. Serikali imeweza kufuta na kupunguza tozo na ada ambazo zilikuwa ni kero katika sekta hizo.
“Nimefurahi kuona bidhaa zinazozalishwa nchini katika sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi zinaubora wa hali ya juu, na hii inaashiria dhana ya viwanda vinavyozalisha nchini vinatumia teknolojia ya kisasa” alisema Mhagama
Aidha alitoa wito juu ya utunzaji wa mazingira, utatuzi wa migogoro ya wakulima, wafugaji na wavuvi, pamoja na viongozi na watendaji kushirikiana katika kutambua makundi ya vijana wenye viwango mbalimbali vya ujuzi na elimu, ili waweze kujifunza kupitia maonesho hayo, vilevile watengenezewe mfumo wa kuwabadilisha fikra kwenye suala la ajira kwa kutumia teknolojia zilizojidhihirisha kwenye maonesho hayo ili waweze kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema kuwa maonesho haya yamekuwa na manufaa kwa kuwahamasisha wakulima, wafungaji na wavuvi kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vilivyoanzishwa hapa nchini.