Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 10:55 pm

NEWS: WAZIRI LUGOLA AWASHUKIA WAKURUNGEZI WA HALMASHAURI NCHINI.

DODOMA: Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola amewaagiza wakurrungenzi wa halmashauri zote nchini kushirikiana na jeshi la zimamoto kuhakikisha wanatenga fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya jeshi hilo na si kuitegemea serikali kuu peke.

Waziri Kangi amesema hayo wakati akifungua maadhimisho ya mwaka ya siku ya zimamoto kitaifa yaliyofanyika leo jijini Dodoma .

Amesema uhaba wa vifaa katika jeshi hilo hautamalizika kama serikali kuu pekee ndiyo inayotegemewa hivyo wakurugenzi wa halmashauri katika maeneo yao wanapaswa kutenga fedha.

Waziri Kangi pia amesema serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 208/2019 itatoa ajira 1500 kwa Askari wa zimamoto ili kuondoa tatizo la upungufu wa askari hao huku ikitenga kiasi cha shilingi billion 4.5 kwaajili ya jeshi hilo.

Awali akiwasilisha taarifa Kamishna Jenerali wa Zimamoto nchini Thobias Andengenye amesema matukio ya moto yamepungua nchini kwani katika mwaka wa fedha 2016/2017 matukio hayo yalikua 1614 huku 2017/2018 matukio ya moto yapo 1529.