Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:26 am

News: Waziri Lugola aagiza vigogo wanne kunaswa


DOM: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini DCI kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa NIDA Dickson Maimu pamoja na watumishi wengine wa NIDA waliohusika katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na kisha kuwapeleka katika Mahakama ya mafisadi.

Lakini pia Waziri Lugola ameamuru kukamatwa kwa wadhabuni watatu walioshindwa kurejesha fedha wanazodaiwa na Serikali ambapo nao wataunganishwa katika Mahakama hiyo ya mafisadi.

Lugola pia ameagiza kukamatwa kwa wamiliki wa kampuni tatu zinazodaiwa kuhusika katika mradi wa vitambulisho vya taifa, Gotham's International Limited, Gwiholoto Impex Ltd na Aste Insurance wanaodaiwa kufanya udanganyifu na kushindwa kurejesha fedha walizotumia kinyume na utaratibu.

Akizungumza na wanahabari leo Agosti 21, Lugola ameagiza kukamatwa watumishi wote wa Nida ambao wanatuhumiwa katika ubadhirifu wa fedha za umma wakishirikina na kampuni hizo.

“Hizi kampuni zimefanya udanganyifu zikishirikiana na baadhi ya wafanyakazi,”amesema.