Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:10 am

NEWS: WAZIRI KALEMANI APIGA MARUFUKU MGAO WA UMEME NCHINI

Waziriwa wa nishati nchini Tanzania Dkt Medard Kalemani amepiga marufuku kwa
uongozi wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO kwa kitendo chao cha kutoa nishati ya umeme kwa mgao wakati hakuna tatizo lolote la uzalishaji katika vituo vyote vitatu.

Akizungumza wakati wa ziara katika kituo cha uzalisha ji wa umeme Mtera mkoani iringa,Dkt Medard Kalemani alisema kuwa “haiwezekani mtu mmoja anaamua kutoa maagizo ya kuwepo mgao wakati hakuna tatizo lolote lile”.

Alitoaagizo hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba Kuhakikisha anamchukulia hatua mfanyakazi aitwae Abubakari kwa kosa la kuagiza mkoa wa Mwanza kuwepo kwa mgao wa umeme bila sababu za msingi.

"Usipomchukuliahatua huyu mfanyakazi anaeitwa Abubakari basi Mimi nitajua nani wa kumchukuliahatua kwa kuwa tatizo hilo kwa Abubakari limekuwa likijirudia mara kwa mara"alisema

Alisemaserikali imejenga nyumba za wafanyazi pale ubongo kwa ajili ya uangaliangalizi wa mwenendo wa umeme nchi nzima lakini bado wafanyakazi wanakaidi kukaa hapo jambolinalopelekea ufanisi wa kazi kuwa hafifu.

AliwaagizaMameneja wa TANESCO mikoa yote hapa nchini kuhakikisha wanawasimamia vilivyowafanyakazi wengine ili watimize wajibu wao katika kutimiza ahadi ya kutoahuduma ya nishati kwa wananchi.

AidhaDkt. Medard Kalemani alitoa tahadhari kwa wananchi
waliokaribu na mto Ruaha mkuu kuchukua tahadhari kwa kuwa wameamua kufungulia maji kutoka katika bwawa la Mtera na Kidatu kutokana na kujaa hadi kupitiliza kiwango kinacho hitajika.

Alisema Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari na kuongeza kuwa maji hayatakuwa yanasambaa bali yatapita kwenye mkondo wake wa asili ambako wananchi wanafanya shughuli zao za kijamii.

"TANESCO tumeona ni muhimu kutoa tahadhari kwa Wananchi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, kwa kawaida Bwawa la Mtera kulijaza huchukua miezi 3 hadi 4 kwa mvua za masika, lakini kwa kipindi hiki mvua za vuli zimekuwa nyingi ndani ya mwezi mmoja hivyo kina kimeongezeka", alisema

Alisema tahadhari inatolewa kwa Wananchi kusitisha shughuli zao za kijamii kama uvuvi, kulisha mifugo, kilimo na nyingine kwenye mkondo wa maji au sehemu zenye vidimbwi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Aliongezakuwa, kawaida kina cha maji kujaa ni mita 698.50 juu ya usawa bahari na kuongeza hivi sasa kina cha maji kimefikia 698.03 juu ya usawa wa bahari.