Home | Terms & Conditions | Help

January 10, 2025, 2:28 pm

NEWS: WAZIRI KABUDI APOKEA TAARIFA YA VAZI LA TAIFA

DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi amepokea taarifa maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kutoka kwa kamati iliyoundwa kwa ajili ya maandalizi ya vazi hilo.

Waziri Kabudi amesema mchakato wa vazi la Taifa umeanza kuwa na mafanikio kutokana na jitihada zilizofikiwa kwa sasa ambapo kamati imewasilisha taarifa maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kwa Wizara yake.

Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akipokea taarifa hiyo maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kutoka kwa kamati maalumu ya uandaaji wa vazi hilo.

Kabudi amesema, ili kupata vazi la Taifa ni mchakatu wenye hatua tofauti na sio suala la mara moja bali ni lazima lipate maoni ya wananchi na wadau mbalimbali ambapo michoro hoyo iloyopendekezwa itachapishwa ili kila mmoja aikne na maoni yake.