- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI JAFO ATOA SIKU 30 KWA WAKUU WA MIKOA KUKAMILISHA TAKWIMU
Dodoma: Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo amewapa mwezi mmoja tu wakuu wa mikoa wote nchini kukamilisha sensa ya wazee katika mikoa yao. Jafo ameagiza wakuu hao kuwashughulikia watendaji wote katika maeneo yao watakaokwamisha zoezi hilo.
Akizungumza na waandishi leo May 28 Jijini Dodoma, amesema Serikali inafanya sensa ili kuwatambua wazee waweze kuwapa huduma stahiki. "Tunatambua kuwa wazee wametoa mchango mkubwa katika taifa hili katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini asilimia 75 ya wazee wanaishi vijijini wengi wakiwa wanawake hawapati huduma stahiki," amesema Jafo.
Ameagiza zoezi hilo kufanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na itakapofika Juni 30 taarifa ziwe zimefika Tamisemi na wazee hao wawe wamepewa vitambulisho maalumu kwa ajili ya kupatiwa huduma.