- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI JAFO ASHTUKIA JANJA JANJA YA DC KILOSA, NAKUMTAKA KUANDIKA BARUA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Sulemani Jafo ameshtukia uwongo aliotaka kufanyiwa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa akiwemo mkuu wa wilaya hiyo kwa kumdanganya kuwa ujenzi unaendelea katika kituo cha Afya Mikumi licha ya kupokea fedha hizo mapema tangu mwishoni mwa mwezi June 2018.
Katika ziara hiyo ya kushtukiza watendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilosa inaonekana walidamka asubuhi ya leo na kupeleka mchanga zaidi ya Maroli sita pamoja na fundi aliyekuwa akichanganya mchanga huo ili ionekane kazi inaendelea lakini waziri Jafo aligundua janja hiyo na kutoa maagizo mazito kwa Uongozi wa Halmashauri hiyo. ‘
Niwatake Mkurugenzi wa Kilosa, Mweka Hazina, Mkanga Mkuu wa Wilaya, Afisa Mipango pamoja na Mhandisi kuwasilisha barua zenu haraka sana Ofisi ya Rais Tamisemi za kujieleza kwanini msichukuliwe hatua kutokana na uzembe mlioufanya katika kituo hiki’ aliagiza Jafo.
Aliongeza kuwa Mpaka sasa kituo hikinwapo katika hatua ya msingi wakati wenzao wa maeneo mengine waliopewa fedha wakati mmoja wakiwa katika hatua za umaliziaji. Ziara hiyo ya waziri Jafo Mkoani Morogoro amefanikiwa kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Mikumi, ujenzi wa kituo cha afya Kidodi, pamoja na kutembelea eneo la Luhembe ambapo patajengwa daraja kubwa litakalo gharimu zaidi ya shilingi milioni mia nane.