- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI ALIYEHAMIA CHADEMA ATOA SIRI YA KUSHAWISHIWA KURUDI CCM
Dar es salaam: Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Dk Makongoro Mahanga aliyetoka CCM na kutimkia CHADEMA mwaka 2015 amedai kushawishiwa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makongoro Mahanga katikati akiwa na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa
Akiongea leo Jumapili Desemba 3,2017 na gazeti la mwananchi Dk Makongoro amesema mara kwa mara amekuwa akifuatwa na watu tofauti wakiwamo ndugu zake wakimshawishi arejee kwenye chama hicho tawala.
Amesema, “Nawaambia hivi sirudi huko. Huwa nina ishi kwa ninachokiamini na hakuna kinachoweza kunishawishi kubadili imani na dhamira yangu ya Agosti 2 mwaka 2015.”Awali, kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook Dk Mahanga aliwataka wahusika kuacha kuwatuma rafiki zake na ndugu zake ili kumshawishi kurejea CCM.
“Imani yangu, utu wangu na msimamo wangu huwa hauna bei. Kamwe sitorudi CCM acheni kuhangaika,” amesema Dk Mahanga katika ukurasa huo.
Dk Mahanga alihama CCM Agosti 2,2015 baada ya kushindwa katika kura ya maoni kwa nafasi ya ubunge jimbo la Segerea.
Mbunge huyo wa zamani wa Segerea alijitoa CCM akisema ni kwa sababu utaratibu uliotumika haukuwa sahihi na uligubikwa na vitendo vya rushwa na njama zilizofanywa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho tawala.