- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI ALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA TAARIFA SAHIHI JUU YA AJALI WATUMISHI WA SEREKALI
Singida: Waziri wa kilimo na Chakula Dkt. Charles Tizeba ameliangiza jeshi la polisi mkoa wa Singida kufanya uchunguzi upya wa chanzo cha ajali ya watumishi wa tano wa Wizara hiyo iliyotokea Oktoba 21 wilayani Manyoni mkoani humo, kwamaana kuwa taarifa waliyoitoa awali haiendani na uhalisia wa ajali hiyo.
Dkt Tizeba amesema jeshi hilo linapaswa kutoa taarifa sahihi kulingana na tukio lenyewe kwani mijadala inayoendelea juu ya tukio hilo sio sahihi.
Juzi Octoba 21 Watu watano walifariki dunia katika ajali iliyohusisha gari dogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula na lori iliyotokea eneo la Njirii Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Gari dogo lilikuwa limebeba wataalam wanne pamoja na dereva, wote walifariki palepale.