- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI AJIFANYA ABIRIA KITUO CHA MABASI UBUNGO, BAADA YA ZIARA YA KUSHTUKIZA
Dar es salaam: Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amefaya ziara ya kushtukiza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo Jijini Dar es salaam na kuona hali ya usafiri akiwa kama abiria ambapo hata yeye alipewa nauli mpya katika tiketi yake ambayo haiko katika bei elekezi.
"Nimefika kitoni hapo saa 11:15 alfajiri nakuzunguka kwenye baadhi ya mabasi na kubaini baadhi ya abiria kulipishwa nauli tofauti na bei elekezi ya Serikali,"amesema Mhandisi Kamwelwe.Amesema baada ya ukaguzi amebaini abiria kulipa nauli tofautitofauti inatokana na kuwepo kwa madalali nje ya kituo.
Hali ya sasa ya usafiri katika kituo hicho hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka inaonekana kubadilika kutokana na nauli kupandishwa kiholela bila kufuata utaratibu was Serikali.
Hivyo amesema kuna haja ya kupeleka mapendekezo bungeni ili kuwepo kwa tiketi za mfumo wa kieletroniki zitakazosaidia kuondokana na ulanguzi unaoumiza abiria.Baadhi ya abiria wamesema kinachosababisha nauli ipande ni madalali wanaokatisha tiketi nje ya kituo.
Mmoja wa abiria Joseph Malisa amesema unapoenda kwenye ofisi au gari husika unaambiwa gari limejaa lakini nje ya kituo unakuta madalali wanauza tiketi za basi hiyo waliodai kuwa imejaa."Unapofika kwenye gari au ofisi zao unaambiwa nafasi zimejaa lakini nje ya kituo madalali wanauza tiketi kwa bei ya juu na mimi nataka kusafiri inanililazimu kukata bei ya juu" amesema Malisa.
Abiria nwingine Emili Msuya amesema kupanda kwa nauli kiholela kumechangiwa na watu wasio rasmi ikiwemo wapiga debe wanaolundikana ndani ya kituo, hivyo Serikali iangalie utaratibu wa kuwaondoa.Meneja wa Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam Imani Kasagala amesema mabasi yote yanapaswa kuingia ndani ya kituo cha mabasi Ubungo badala ya wamiliki kupaki nje na kutafuta madalali ambao ndio chanzo cha kwa nauli hizo kupanda.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhan Kailima amesema kuwa abiria wakiona kuna kupandishiwa nauli wanatakiwa kutoa taarifa.Amesema mabasi yote yanakaguliwa na kupongeza Ukaguzi unaofanywa katika kituo hicho.