Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:41 am

NEWS: WAZIRI AFAFANUA SABABU YA TAIFA STAA KUTOSAFIRI NA DREAMLINER

Dar es salaam: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrisoni Mwakyembe amefafanua sababu zilizopeleke Dreamliner kushindwa kuisafirisha timu ya taifa ya Mpira wa miguu (Taifa Staa) kwenda Cape Verde kama ambavyo ilitangazwa awali.

" Zilianza kusambaa taarifa kwenye mitandao kwamba ndege kubwa ya Tanzania Dreamliner ambayo ilipangwa kusafirisha wachezaji pamoja na mashabiki kwenda Cape Verde, haitaweza kutua kwenye mji mkuu wa visiwa hivyo Praia kutokana na udogo wa kiwanja cha ndege (ukubwa wa njia ya kuruka na kutua)

Waziri Mwekyembe ametoa kauli hiyo Leo October 9, 2018 wakati akiongea na Waandishi wa Habari nakuesema kuwa Taarifa hizo walizipata jana usiku na kuwalazimu kuzifanyia kazi mara moja kwa kuwasiliana na mratibu wa taifa Stars Alhaj Mgoyi ambaye walimtanguliza huko kutufanyia maandalizi mbalimbali."

"Vilevile tuliwasiliana na wenzetu Air Tanzania idara yao ya ufundi, wakathibitisha kiwanja cha ndege cha Praia ni kidogo njia yake ina urefu wa KM 2.1 wakati Dreamliner inahitaji kiwanja chenye urefu si chini ya KM 3 iweze kutua na kuruka."

"Wenzetu wa ATC walikuwa wanajua lakini wakasema si lazima kutua Praia, kuna kisiwa kingine (Sal) ni Cape Verde pia ndio chenye viwanja virefu kwa hiyo ndege ingetua Sal, kutola Sal kwenda Praia ni dakika 45."

"Kwetu sisi suala si kuruka na kutua ila ni kuepusha timu yetu isipate usumbufu wowote ule ambao unaweza kuathiri perfomance ya timu yetu. Usumbufu unaweza kuwa wa kawaida au wa kutengenezwa." Aliongea Mwakyembe