- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI AAGIZA WAFANYAKAZI WA BENKI WACHUNGUZWE.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philipo Mipango, amezitaka benki zote nchini kuanza kuwachunguza wafanyakazi wao na wasiowaadilifu ili wachukuliwe hatua. Waziri Mpango amesema lengo la agizo hilo ni kuzijengea benki imani kwa wateja wao.
Aliziagiza benki zote kufanya uhakiki na kuwachunguza wafanyakazi wao wote ili kutambua ambao sio waaminifu.
Aidha, ameliagiza Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza matukio ya uhalifu yanapotokea kwenye benki na kwamba endapo wafanyakazi watabainika kupanga njama, uongozi wa benki husika uwachukulie hatua za kisheria.
Waziri Mipango alisema hayo wakati wa ufunguzi wa tawi la Benki ya Amana jijini hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kwa benki zitakazobainika wafanyakazi wake kuhusika katika tukio lolote la wizi wa fedha za wateja.
Dk. Mpango pia alizungumzia matukio ya watu kuvamiwa na kuporwa baada ya kutoka kwenye benki.
Alieleza kuwa matukio ya wateja kuporwa fedha wanapotoka benki ni ya kutisha na kwamba yanatokana na baadhi ya wafanyakazi ambao siyowaadilifu na waaminifu kushirikiana na wahalifu hao.
Alitaka matukio hayo yafike mwisho kwa wafanyakazi kuchunguzwa na kwamba benki ambayo haitafanya uchunguzi kwa wafanyakazi wake na likatokea tukio kama hilo, viongozi wake wawajibike.
Alisema lengo la zoezi hilo ni kujenga imani kwa wateja kwa kuwa matukio hayo yanawafanya kuona benki siyo mahala pa siri na si salama tena kwa usalama wao na mali zao.