- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI AAGIZA KUONDOLEWA KWA MITA ZOTE ZA UMEME ZA ZAMANI NCHINI
SONGWE: Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo kuondoa mita zote za umeme nchini ambazo wateja hufanya malipo baada ya kutumia umeme (Conventional Meters) ifikapo mwezi june mwaka huu.
Dkt.Kalemani aliyasema hayo wilayani Ileje mkoani Songwe wakati akizungumza na Mkuu wa wilaya hiyo, Joseph Mkude, Mbunge wa Ileje, Janet Mbene, Watendaji wa TANESCO Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Wizara ya Nishati, na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kabla ya kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu katika Wilaya husika.
Alisema kuwa, jumla ya wateja Laki Tatu (300,000), katika nchi nzima hutumia mita hizo za zamani huku wateja 48,000 wakiwa wanatumia conventional meters ambazo muda wake umeisha. " Kuendelea kutumia mita hizi ni kupoteza mapato ya Shirika, kwa mfano hawa wateja 48,000 wanatumia umeme bila sisi kujua wametumia kiasi gani, hivyo nawaagiza kuwa, mwisho wa kutumia mita hizi ni mwezi Juni na wateja wote wafungiwe mita mpya za umeme ili Serikali ikusanye mapato yake ipasavyo," alisema Dkt Kalemani.
Pia Dkt. Kalemani aliwaagiza Mameneja wa TANESCO nchini kuhakikisha kuwa kazi ya kufanya marekebisho mbalimbali katika miundombinu ya umeme ikiwemo uondoaji wa nguzo zilizochakaa iwe imekamilika kabla ya mwezi Juni mwaka huu kwani fedha za kufanya kazi husika zilishatolewa.
Akizungumzia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III), Dkt. Kalemani alisema kuwa, mradi huo unaolenga kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini, utakamilika mwezi Juni mwaka 2021 ambapo lengo ni kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wawe wameunganishwa na huduma ya umeme kufikia mwaka huo. Waziri wa Nishati, pia aliwaagiza watendaji wa TANESCO, REA na Wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kuhakikisha kuwa vijiji vyote ambavyo vilipitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina umeme.
visambaziwe nishati hiyo kupitia mradi wa REA III mzunguko wa kwanza unaokamilika mwezi Juni, 2019. Vilevile, alitoa wito kwa Halmashauri zote pamoja na Serikali za Vijiji nchini, kutenga fedha zitakazosaidia Taasisi za Serikali katika maeneo yao kama vile Shule na Vituo vya Afya kuunganishwa na huduma ya umeme ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi