Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:46 am

NEWS: WAZIRI AAGIZA KUFUTWA HATI WANAOMILIKI MAENEO KARIBU NA AIRPORT

Arusha: Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kufuta hati za umiliki wa ardhi za kampuni za Puma Energy na Tanzan air zilizopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Agizo hilo amelitoa baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Nditiye amasema haiwezekani kampuni binafsi kuwa na hati za kumiliki ardhi katikati ya uwanja wa ndege wa Serikali.

"Hati hizi zinapaswa kufutwa haraka sana na hizi kampuni zinapaswa kupangishwa katika uwanja huo, kuna madhara makubwa mtu binafsi kuwa na hati katikati ya uwanja, anaweza kuchukua mkopo katika benki na akashindwa kulipa je itakuwaje?" amehoji.

Amesema TAA inapaswa kuhakikisha inalifikisha suala hilo Wizara ya Ardhi na taasisi nyingine za Serikali ili hati hizo zifutwe.

Amesema haiwezekani Rais John Magufuli anautangaza uwanja wa JNIA kuwa ni mali ya Serikali kumbe katikati kuna watu binafsi.