- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZAZI WAPAGAWA KWA MAADILI BORA KWA WASICHANA.
Wakibubujika kwa furaha baada ya kuwaona wasichana wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria De’Matias inayomilikiwa na madhehebu ya Kanisa Katoliki mjini Dodoma wakati wa mahafali ya kadato cha Nne shuleni hapo siku ya jumamosi iliyopita October 21, wamesema wanaimani kubwa na shule hizo.
Mwakilishi wa wazazi na walezi hao alipopatiwa nafasi ya kuongea kwa niaba ya wengine Madam Elieshi Mfangavo kutoka Dar es Salaam alisema, hawawezi kujizuia kuonyesha furaha yao ilivyo kubwa kwani wamepagawa na kufarijika mno wanapowaona mabinti zao wakiwa katika hali ya nidhamu.
Mzazi huyo Madam Mfangavo huku akinukuu maneno kutoka katika sehemu ya kitabu cha maandiko matakatifu cha Bibilia, Zaburi ya 126:2 kinachosema “ Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimu wetu kelele za furaha” .
Akitoa hotuba yake ya pongezi kwa shule hiyo kwa niaba ya shule zote za madhehebu ya dini kwa kazi nzuri wanayofanya kuisaidia serekali kuwalea vizuri wanafunzi hususani wa kike, Mkurugenzi huyo pia alizishauri shule hizo za madhehebu ya dini zisijifungie zenyewe bali zishirikiane na shule zingine za umma na zile za binafsi kueneza mambo mazuri wanayofanya wao.
Madam Lyimo alifafanua zaidi kwa kusema kwamba “sera nzuri ya elimu iliyopitishwa na serikali ndio msingi pekee kwetu, kutuwezesha kutoa elimu yenye kukidhi haja ya sasa kwa wazazi na walezi kwa wanafunzi hawa vinginevyo tusingeweza” alisema.
Amewataka wazazi na walezi wenye mabinti zao katika shule hiyo wawe tayari kuwapokea watoto wao mara baada ya kumaliza mitihani yao ya mwisho ya kaidato cha Nne ambapo amesema wapo katika kiwango cha juu cha kitaaluma, kimaadili na nidhamu hivyo wasikubalike wabadilike.
Shule hiyo ni ya wasichana pekee kuanzia chekechea hadi kidato cha sita na watakaofanya mitihani ya kidato cha Nne kuanzia October 30 wapo 63.