- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAWILI MBARONI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA SEREKALI
Mwanza: Jeshi la polisi jijini Mwanza linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa Serikali na kuwatapeli wananchi fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 6,2018 Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Jonathan Shanna amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 3, 2018 saa saba mchana Mtaa wa Nyegezi Stendi jijini Mwanza na walifanikiwa kuwatia mbaroni baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.
amewataja watuhumiwa hao ni Elias Malelemba (47) mkazi wa jijini Dar e s Salaam na Sharifu Hamis (58) mkazi wa Mkarama Singida.
“Watuhumiwa waliwatapeli watu wawili Sh160, 000 huku wakiendelea kudai Sh1 milioni ili wawapatie nafasi watoto wao ya kwenda kwenye mafunzo ya uaskari katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (CCP) na mwingine chuo cha udaktari cha Haidom mkoani Manyara,” amesema Shanna