Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:50 am

NEWS: WATU WANNE WAMEJITOKEZA KUPIGA USHINDI WA RAIS KENYATTA

Nairobi: Watu wanne wamewasilisha malalamiko yao kwenye Makahakama ya Juu nchini Kenya wakipinga ushindi wa Uhuru Kenyatta na kudai kuwa uchaguzi huo haukufuata sheria na Misingi ya katiba ya Kenya.

Watu walio wasilisha malalamiko yao ni Mbunge wa zamani Harun Mwau, ambaye, amesema wakati Mahakama Kuu ilifuta uchaguzi wa Agosti 8, mchakato wa uchaguzi ungelianza upya.

Wanaharakati wawili wa haki za binadamu, Khalef Khalifa Njonjo Mue, walitoa malalamiko yao dhidi ya Tume ya Uchaguzi (IEBC) wakiishtumu kutowajibika kwa majukumu yao, upendeleo, ukiukwaji wa sheria na udanganyifu. Aidha, kwa mujibu wa wanaharakati hao, IEBC haingepaswa kuandaa uchaguzi katika mazingira ya machafuko wakati ambapo ilijua kwamba majimbo 25 hayangeliweza kushiriki kura hiyo.

Shirika linaloitwa Black Flag pia limewasilisha malalamiko yake kwenye Mahakama Kuu dhidi ya IEBC, Uhuru Kenyatta lakini pia dhidi ya Raila Odinga.

Hatimaye, shirika linalotetea Utawala wa Kidemokrasia (Institute Of Democratic Governance) limeanzisha utaratibu dhidi ya viongozi wa upinzani watano, ikiwa ni pamoja na Raila Odinga. shirika hili linawashtumu vongozi hao wa upinzani kuwasababisha vurugu za uchaguzi na kuomba wafunguliwe mashitaka.


Mnamo mwezi Agosti, uchaguzi wa urais ulifutwa na Mahakama Kuu, na kupelekea uchaguzi mpya kufanyika Oktoba 26. Rais Kenyatta alichaguliwa tena. Siku ya Jumatatu, Novemba 6, wakati ambapo ilikuwa ni tarehe ya mwisho wa kuwasilisha malalamiko mahakamani kuhusu uchauzi huo.