- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU WAJITOKEZA KUPIMA TEZI DUMA MUHIMBILI
Dar es salaam: Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo November 3, 2018 wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya zoezi la kupima bure tezi dume (prostate) na mfumo wa njia ya mkojo kwa kutumia ultrasound.
Zoezi hilo limeandaliwa na Hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Matumizi ya Mionzi katika uchunguzi na Tiba Tanzania (TARA) ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya wataalam wa mionzi tiba duniani.
Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia, Dkt. Lulu Sakafu amesema umri unavyozidi kwenda juu, wanaume wanakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, hivyo wameshauriwa kujenga utamaduni kwa kupima afya zao mara kwa mara.
Amesema watu wasiofanya mazoezi wako katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, wanaume wanaopenda kula chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta na wengine wanaweza pata ugonjwa huo kutokana na historia ya familia zao.
“Katika maadhimisho ya mwaka huu tumeamua kupima tezi dume kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 ili kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa huu kwa sababu kansa ya tezi dume duniani inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo kwa wanaume kutokana na saratani ya tezi dume,” amesema Dkt. Sakafu.