- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WATU SABA WAUAWA KATIKA MAPAMBANO YA WAASI NA ASKARI WA KONGO
7 wauawa katika makabiliano baina ya askari na waasi Kongo DR
watu saba wameuawa katika makabiliano ya risasi kati ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi moja la waasi, katika mkoa wa Kivu Kusini.
Duru za habari zimesema raia wawili ni miongoni mwa watu waliouawa katika makabiliano hayo yaliyoanza Jumapili iliyopita na kuendelea hadi jana Jumatatu.
Wanajeshi wa Kongo DR wamekabiliana vikali na wafuasi wa aliyekuwa kamanda wa ngazi za juu aliyeasi jeshi katika mji wa Bukavu, mashariki mwa nchi hiyo ambaye baadaye alijisalimisha kwa askari wa Kikosi cha Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, katika mji huo.
Msemaji wa Jeshi la Kongo katika eneo la Kivu Kusini Dieudonne Kasereka amesema mapigano yalianza pale polisi walipotaka kumpokonya silaha Kanali Abbas Kayonga, ambaye alifutwa kazi Alkhamisi iliyopita.
Kasereka amesema kamanda huyo wa zamani wa jeshi la DRC amejisalimisha akiwa pamoja na wafuasi wake 17.
Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa miongo kadhaa sasa limekuwa kitovu cha mapigano kutokana na utajiri wake wa madini.