Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:47 am

NEWS : WATU SABA WAMEFARIKI NA WENGINE 20 KUJERUHIWA BAADA YA KUTOKEA SHAMBULIZI AFRIKA YA KATI

Watu 7 wauawa na 20 wajeruhiwa Jamhburi ya Afrika ya Kati

Watu 7 wauawa na 20 wajeruhiwa Jamhburi ya Afrika ya Kati

Habari kutoka Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) zinasema kuwa watu saba wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya kutokea shambulizi la guruneti katika eneo la starehe na katika machafuko ya ulipizaji kisasi siku mbili mfululizo mjini humo.

Mashambulizi hayo yametokea huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kulipigia kura azimio lililopendekezwa na Ufaransa kuhusu kutumwa wanajeshi 900 wa ziada kwa ajili ya kuwalinda raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wiki hii. Mwaka 2013 mji wa Bangui ulikumbwa na machafuko mabaya ya kidini baina ya Waislamu na Wakristo na tangu wakati huo hadi hivi sasa hali haijarejesha katika mazingira yake ya kawaida.

Magaidi wa Kikristo wa Anti-Balaka wakimfanyia istihzai Muislamu kabla ya kumpiga visu na kumuua katika machafuko yaliyoikumba CAR mwaka 2013

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Henri Wanzet Linguissara, amesema kuwa, watu wawili waliokuwa wamepanda pikipiki walikwenda karibu na mkusanyiko wa watu waliokuwa katika burudani ya muziki iliyoitishwa jana usiku kwa lengo la kuhimiza maelewano na amani nchini humo na kurusha guruneti katikati ya kundi la watu.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Simplice Mathieu Sarandji, amewataka wananchi wa nchi hiyo kuwa watulivu na kujiepusha na machafuko. Mapigano makali ya kutumia silaha yalitokea katika eneo lenye Waislamu wengi baada ya shambulio hilo.

Machafuko yanaendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya kuweko wanajeshi 12,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Wiki ijayo, Baraza la Usalama la umoja huo linatarajiwa kup[igia kura pendekezo la Ufaransa la kutumwa wanajeshi 900 zaidi wa kulinda amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.