Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 3:41 am

NEWS: WATU KADHAA WAUAWA KATIKA MAANDAMANO DHIDI YA SERIKALI YA JAMHURI YA KONGO

Kadhaa wauawa katika maandamano dhidi ya serikali Kongo DR

  • Kadhaa wauawa katika maandamano dhidi ya serikali Kongo DR

Kwa akali watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika ghasia za maandamano dhidi ya serikali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa Ida Sawyer, Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika eneo la Afrika ya Kati, waandamanaji hao wameuawa na maafisa usalama hii leo nje ya Kanisa la Kikatoliki la St. Alphonse, katika wilaya ya Matete, viungani mwa mji mkuu Kinshasa.

Maafisa wa usalama wamefyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi kuwatawanya waumini wa Kanisa Katoliki waliokuwa wanaendelea na ibada jijini Kinshasa siku ya Jumapili, ambapo baadaye walitazamiwa wamiminike mabarabarani kushiriki maandamano hayo.

Watetezi wa haki za binadamu wamesema watu 50 wamekamatwa mjini Kinshasa, huku wengine 25 wakikamatwa katika mji wa Kamina.

Waandamanaji kadhaa wametiwa nguvuni

Hata hivyo, msemaji wa polisi nchini humo, Pierrot Mwanamputu amekanusha madai kuwa maafisa usalama wametumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano hayo.

Polisi ya Kongo DR hapo jana ilipiga marufuku maandamano hayo ikisema kuwa sio halali, mbali na vyombo vya usalama kufunga intaneti kwa lengo la kuzuia mawasiliano kwenye mitandao ya kijamii.

Kabila yuko madarakani tangu mwaka 2001