- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 6 WAUWAWA KWA RISASI NCHINI KENYA
Kenya: Watu sita ikiwa ni pamoja na wanafunzi watano na mlinzi mmoja wamepigwa risasi na kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya katika shambulio lililotokea asubuhi jana 14 Octoba dhidi ya shule ya upili ya Lokichogio,Kaskazini mwa Kenya, karibu na mpaka wa Sudan Kusini.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo anasema kuwa mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo aliyefukuzwa kwenda shuleni baada kupigana na mwenzake ni miongoni mwa washambuliaji.
Aliagizwa kurudi na wazazi wake lakini hakufanya hivyo.
Mashahidi wanasema watu watatu waliokuwa na silaha, mmoja wao akiwa mwanafunzi wa zamani walivamia mabweni katika Shule ya Upili ya Lokichogio mapema asubuhi.
Lokochogio iko karibu na mpaka wa Sudan Kusini na Ethiopia na wakaazi wengi wa eneo hilo hubeba bunduki na ni wachungaji wanaolinda mifugo wao dhidi ya wizi.
Walioshuhudia walisema kuwa mwanafunzi huyo alirudi shuleni usiku wa manane na wenzake wawili.
Inaarifiwa kuwa mwanafunzi huyo hakuwa shuleni wakati huo na washambuliaji hao waliwapiga risasi na kuwaua wanafunzi watano na kuwabaka wasichana wawili.
Inadaiwa kuwa walimpiga risasi na kumuua mlinzi na kisha kwenda katika mabweni wakimtafuta mwanafunzi waliyepigana naye awali.
Mwanafunzi huyo hakuwa shuleni wakati huo na washambuliaji hao waliwapiga risasi na kuwaua wanafunzi watano na kuwabaka wasichana wawili.
Viongozi mbalimbali nchini Kenya wamelaani mauaji hayo ya kinayama, polisi imekua ikiwasaka wahalifu.