Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:37 am

NEWS: WATU 46 MBARONI DODOMA.

DODOMA: Jeshi la polisi mkoni Dodoma linawashikilia watuhumiwa 46 wa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na nyara za serikali zenye dhamani ya zaidi ya shilingi million 20.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni hiyo iliyofanywa kuanzia oct 4 hadi 12 mwaka huu ikihusu taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika na umeme nchini (TANESCO), Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA), Uhamiaji, Maliasili na Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amesema kuwa katika moparesheni hiyo zimekamatwa nyara za serikali ambazo ni ngozi mbili za mnyama aina ya chuwi zenye thamani y ash. 15,750,000, nyama ya mnyamapori aina ya tandara kilogram tatu zenye thamani ya sh. 5,700,000 ambapo hapa kamanda anabanisha makosa mengine.

Katika operesheni hiyo Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limekamata pikipiki tano za wizi pamoja na pikipiki zaidi ya 500 zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.

Amesema mazao ya misitu kamanda amesema kuwa walikamata mbao 200, mkaa pamoja na kamosa ya kuharibia misitu na kufanya shughuli za kuchoma mkataa katika maeneo ya hifadhi.

Hata huvyo amesema tabia ya wazazi kuingia mkataba na dereva bodaboda kupakia watoto kuwapeleka shulengi na kuwarudisha nyumba kamanda Muroto akawataka waalimu kutowapokea wanafunzi wanaotumia usafiri huo.

Oparesheni hiyo pia ilishirikisha mataiafa wanachama wa shirikisho la polisi Afrika mashariki na kusini mwa afrika(EAPCCO na SARPCCO) chini ya shirikisho la polisi Interpol lengo likiwa ni kukabili hali ya uharifu wa makosa mtambuka yanayovuka mipaka ya nchi.