Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:54 pm

NEWS: WATU 22 WAMETEKETEA KWA KEMIKALI NCHINI CHINA

Takriban watu ishirini na mbili wamefariki Dunia na wengine 22 kujeruhiwa na kuteketea kwa Magari zaidi ya 50 baada ya mlipuko wa lori lililokuwa limebeba bidhaa za kemikali mbele ya kiwanda cha Hebei Shenghua Chemical Group cha nchini China.

Tukio hilo limetokea leo siku ya Jumatano katika mji wa Zhangjiakou, mji ambao unakusudiwa kupokea mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi mnamo mwaka 2022, kwa mujibu wa viongozi na vyombo vya habari nchini China.

Malori 38 na magari 12 yameharibika kutokana na mlipuko huo kufuatia kuzuka kwa moto mbele ya kiwanda hicho katika mji wa Zhangjiakou, kilomita 200 kaskazini magharibi mwa Beijing, manispaa ya mji huo imetangaza kwenye mtandao wa kijamii wa Weibo.

Watu waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali baada ya mlipuko huo uliotokea saa 00:41 saa za China (sawa na saa 10:41 siku ya Jumanne saa za kimataifa), taarifa hiyo imesema.

Tukio hilo lilitokea kwenye lango la kiwanda, wakati gari lililobeba bidhaa hatari lililipuka, na kusababisha magari kadhaa kuharbika, shirika la Habari la China News limesema, likinukuu manispaa ya jiji la Zhangjiakou. Televisheni ya serikali CCTV imesema gari lililolipuka lilikua "lori la mafuta".