Akizungumza na Muakilishi Media kwa njia ya simu Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea Jumapili Agosti 5 na kuwataja waliofariki kuwa ni Bisaku Chacha (19) na Charles Mairo (18).
Amesema marehemu waliingia kwenye shimo lililokuwa limeachwa kwa siku nyingi wakitafuta mawe ya dhahabu matokeo yake waliangukiwa na mawe hayo.
Mzazi wa Charles, Mairo Wembe amesema hakuziamini taarifa za mwanae kufariki dunia, baada ya kurejea nyumbani ndio aliamini.