Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:42 am

NEWS : WATU 15,000 BARANI AFRIKA NI WAKIMBIZI WA KILA SIKU

Watu 15,000 wanakuwa wakimbizi kila siku barani Afrika

Wakimbizi wa Sudan Kusini

Wakimbizi wa Sudan Kusini

Taasisi moja ya barani Ulaya inayoshughulikia masuala ya wakimbizi imetangaza kuwa, katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka jana 2017, kila siku watu 15,000 walikuwa wakikimbia makazi yao barani Afrika.

Taasisi hiyo ya NRC imenukuliwa na shirika rasmi la habari la Algeria ikisema kuwa, mambo makuu yanayowafanya watu barani Afrika wakimbie makazi yao ni vita, machafuko na majanga ya kimaumbile ambayo yanatishia usalama wao.

Wakimbizi wa Burundi

Kwa mujibu wa taasisi hiyo ya Ulaya, nchi zenye wakimbizi wengi zaidi barani Afrika ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nigeria na Sudan Kusini ambako raia wameathiriwa zaidi na mambo hayo ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika. Kwa upande wa mashariki mwa Afrika, Somalia imetajwa kuwa na wakimbizi wengi ambao wanaokimbia vita na machafuko.

Taasisi hiyo ya kurekodi idadi ya wakimbizi yenye makao yake nchini Norway pia imesema, janga hilo limeyalazimisha mashirika ya kimataifa kuchunguza mbinu mpya za kuzuia sababu zinazowafanya watu hao kukimbia makazi yao ili yakiweza yakabiliane na sababu zenyewe zinazoongeza wimbi la wakimbizi.

Wakati huo huo Joel Millman, msemaji wa shirika la kimataifa la wakimbizi amesema kuwa, mwaka uliomalizika wa 2017, zaidi ya watu 5,376 walipoteza maisha yao wakiwa katika harakati za kuyahama makazi yao.