- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WATU 129 WAFARIKI DUNIA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI IRANI
Watu 129 wafariki dunia katika tetemeko la ardhi magharibi mwa Iran, uokoaji waanza
Watu 129 wametangazwa kufariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi lililoyakumba maeneo ya mkoa wa Kermanshah, magharibi mwa Iran.
Hushang Bazund, Mkuu wa Mkoa wa Kermanshah ameliambia Shirika la Habari la IRIB mapema asubuhi leo kwamba kikosi cha kujitolea cha wananchi kimetumwa kwenda maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo kwa ajili ya opereesheni za uokoaji. Kwa mujibu wa Bazund hadi sasa idadi ya watu waliopoteza maisha ni 129.
Hata hivyo amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa idadi ya wahanga ikaongezeka kutoka na uzito wa tetemeko hilo na ukubwa wa eneo lililokumbwa na janga hilo la kimaumbile. Mkuu wa Mkoa wa Kermanshah amesema kuwa, kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa, karibu helikopta 30 zimetumwa eneo la tukio kwa ajili ya kuwabeba majeruhi. Akishiria kuharibiwa pia baadhi ya vituo vya afya katika tukio hilo, amesema kuwa, majeruhi wengine wamepelekwa katika miji mingine iliyo kando na mkoa huo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, kama ambavyo pia amewataka viongozi wa huduma za kijamii kuzifanyia ukarabati wa haraka sekta muhimu kama vile umeme, maji na gesi za mkoa huo. Wakati huo huo, Abdolreza Rahmani Fazli, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran sambamba na kuashiria sisitizo la Rais Hassan Rouhani la kuandaliwa nyenzo zote muhimu kwa ajili ya kutatuliwa matatizo ya maeneo yaliyokumbwa na tetemeko magharibi mwa nchi, amesema kuwa vifaa na nyenzo stahiki katika mikoa ya jirani na Kermanshah vimetumwa kwenda eneo la tukio.
Kadhalika Abdolreza Rahmani Fazli amelitaka jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kuanzisha hospitali za dharura katika eneo hilo na kuwasaidia mejeruhi. Kituo cha masuala ya ardhi katika Chuo Kikuu cha Tehran kimetangaza kuwa, tetemeko hilo la ardhi la uzito wa 7 kwa kipimo cha rishta, lilitokea majira ya saa 3:05 na sekunde 35 usiku na kuyaathiri maeneo ya mkoa wa Kermanshah na Kurdistan ya Iran.