- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 12 WATIWA MBARONI MMOJA APOTEZA MAISHA.
DOM: Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashilikilia watu 12 wakiwemo viongozi wa serikali ya Kijiji cha Ngomai kilichopo wilayani Kongwa kutokana na kushiriki mgogoro baina ya wakulima na wafugaji uliosababisha mtu mmoja kupoteza maisha.
Watuhumiwa hao ni miongoni mwa watu 21 waliokamatwa na jeshi hilo kwa tuhuma mbalimbali yakiwemo makosa ya jinai,uvunjaji,wizi na kupatikana na bhangi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani humo Gilles Muroto amesema tukio hilo limetokea septemba 20 mwaka huu katika kijiji cha Silale wilayani humo.
Kamanda Muroto amesema jeshi hilo pia linawashikilia watu wanne waliokutwa na noti bandia ambazo ni dola za marekani zipatazo 3,181 zilizotengenezwa kienyeji wanaodai kuwa ni wasanii waigizaji ilhali hawana vibali vinavyowatambulisha kuwa ni wasanii.
Miongoni mwa watuhumiwa 21 wanaoshikiliwa na jeshi hilo yupo mwanafunzi wa Chuo Cha Mipango kilichopo mjini Dodoma James Senya anayetuhumiwa kuwasaidia watu watano kufanya wezi kwa kuwapa taarifa ili wafanye uhalifu.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Muroto amewataka wakazi wa Dodoma kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kuwafichua wahalifu ili Dodoma iendelee kuwa mahali salama huku akiwahimiza wanaomiliki silaha kuhakikisha wanazimiliki kwa mujibu wa sheria.