Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:29 am

NEWS: WATOTO WAWALI WAMEKUTWA WAMESHINJWA NA KUTUPWA KICHAKANI BUKOBA

Bukoba: Taarifa kutoka Mkoani Kagerq zinasema kuwa Watoto wawili wa familia moja wamekutwa wamechinjwa na miili yao kutupwa kwenye kichaka katika Kijiji cha Mashule wilayani hapa baada ya kupotea kwa siku moja.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Isaack Msengi alisema watu tisa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali wamebaini tukio hilo linahusishwa na ushirikina.

Kamanda Msengi alisema Watoto hao, ni Auson Respikius (7) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mashule na Alistidia Respikius (5), waliondoka nyumbani kwao Jumapili iliyopita na miili yao ilipatikana kichakani juzi ikiwa na majeraha shingoni.

Alisema kwa nyakati tofauti familia hiyo imewahi kuchomewa nyumba na wananchi wakishinikizwa wahame eneo hilo, lakini bibi wa watoto hao aliondoka na wajukuu zake na baadaye alirejea kuishi tena kijijini hapo.

“Watoto walikwenda matembezi kwa idhini ya mzazi wao na baadaye walikutwa wamekatwa shingo na kitu chenye makali. Upelelezi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji ni wananchi kuituhumu familia hiyo kwa matendo ya ushirikina,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo, baba wa watoto hao, Respikius John alisema Jumapili iliyopita watoto wake waliomba ruhusa ya kwenda kucheza na baadaye walirejea na kubadili nguo kisha kuondoka tena.

Alisema walipoondoka mara ya pili hawakurejea hadi miili yao ilipokutwa kichakani.

Judith Charles ambaye ni mama mzazi wa watoto hao waliokuwa wakiishi na mama yao wa kambo, alisema alipata taarifa za kupotea kwa watoto wake Jumapili na walianza kuwatafuta lakini hawakuwapata.