- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Watoto 13,600 nchini wanazaliwa na magonjwa ya moyo kila mwaka.
TAKWIMU kutokana Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT) zimeonyesha kuwa watoto 13,600 nchini, wanazaliwa wakiwa na magonjwa mbalimbali ya Moyo.
Kati ya watoto hao, 3,400 wanahitaji kupatiwa matibabu kwa kufanyiwa upasuaji.
Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika, wakati maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani.
“Pia, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) magonjwa yasiyoambukiza yanaua watu milioni 38 duniani kila mwaka.
Ameongeza kwa kusema “Vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo vinakadiriwa kufikia watu milioni 17.5 kila mwaka.
Dk. Chandika amesema magonjwa hayo huenda sambamba na saratani ambayo huua watu milioni 8.2 kwa mwaka huku magonjwa ya njia ya hewa yanaua watu milioni 4 na ugonjwa wa kisukari ukisababisha vifo vya watu takribani milioni 1.5 kila mwaka.
Mbali na hayo amebainisha sababu zinazosababisha magonjwa ya moyo ni kutozingatia kanuni za ulaji wa vyakula bora ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi nyingi, sukari nyingi, uvutaji wa sugara, unywaji pombe kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi.
Dk Chandika amesema katika kuhakikisha hospitali hiyo inatoa huduma bora kwa jamii ikiwemo matibabu ya magonjwa ya moyo, imepata watumishi wapya 94 wakiwemo madaktari na wauguzi.
Amesema hospitali hiyo ina vifaa vya kutosha na inatarajia kuanza kutoa huduma ya kupima magonjwa ya moyo na matibabu baada kupitia maabara maalum.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, alitoa wito kwa Watanzania kujenga tabia ya kupima afya zao na kula mlo kamili.
"Watanzania wengi wamekuwa wakishindwa kupima afya zao huku wakitumia vyakula hatarishi wakiamini kuwa kutumia vyakula vyenye mafuta mengi ni dalili ya uwezo kumbe ni kujiweka Katika mazingira hatarishi,” amesema.
Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa magonywa ya moyo si magonywa ya kitajiri kama baadhi ya watu wanavyoamini bali yanatokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha hususan kutozingatia ulaji bora na kutofanya mazoezi.
“Kuwa na afya bora si unene. Ni matokeo ya kutozingatia ulaji mzuri. Kula mlo kamili hakuitaji kuwa na kipato kikubwa bali hata Mtanzania mwenye kipato kidogo ana uwezo wa kula mlo kamili,” amesisitiza.
Aidha, Odunga alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, ineendelea kuimarisha huduma za afya kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wanapata matibabu bora.