Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:44 am

NEWS: WATENDAJI WALA RUSHWA KUKIONA CHAMOTO.

DOM: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Taifa Gulamhafeez Mukadamu amesema wapo watendaji wabadhirifu wanaojihusisha na rushwa na kwamba kwa sasa wanaendelea na taratibu za kuwabaini ili wachukuliwe hatua.



Aidha amewataka watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakusanya mapato ili ziingie kwenye historia ya ukusanyaji mapato kwa asilimia 100 kama lilivyo jiji la Dodoma.

Hayo yamebainisha leo Wakati akijibu maswali aliyoulizwa Na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ALAT unaotarajiwa kufanyika Septemba 24 hadi 28 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma unaotarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais John Magufuli.

"Ni Kweli wapo watendaji ambao ni wabadhirifu wanajihusisha na rushwa kwenye baadhi ya miradi na kuisababishia kusuasua nilishawaambia wanaotaka kufanya kazi kwa mazoea waachie nafasi ili watu wenye uwezo Na hiari ya kufanya kazi waingie.



Nakiri ni kweli hapa wapo lakini niombe radhi wa wananchi kwamba Serikali inaendelea na utaratibu wa kuwabaini ili wawajibishwe na tukifanya hivyo suala la rushwa litafikia kikomo ,"amesema.

Ameongeza kuwa kuna changamoto kubwa ya matumizi ya Mashine za Kielekroniki za EFD'S ambapo wananchi wengi hawawezi kuzitumia na kuahidi watalifanyia kazi suala hilo

Awali akizungumzia mkutano huo, Mukadamu alisemash.milioni 200 zinatarajia kutumika huku l kauli mbiu katika mkutano huo ikiwa ni Umuhimu wa Mamlaka Za Serikali za mitaa katika kutoa huduma na ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa viwanda.

"Kauli mbiu hiyo ina lengo la kubainisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zipo karibu zaidi na wananchi na zinatoa huduma. Hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu sana katika kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua fursa za uwekezaji na viwanda ili tufikie lengo la kuwa nchi yenye uchumi wa kati,"amesema.



Amesema miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya fedha za Jumuiya, kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Jumuiya kwa mwaka 2018/19.

Kwa upande wake,Meya wa Dodoma Profesa Devis Mwamfupe amesema kufanyika kwa mkutano huo hapa jijini ni fursa kwa wananchi wa hapa kutangaza huduma walizonazo hivyo kuwataka waitumie vizuri maana hapa Ndio kitovu cha sekta za huduma.


"Sekta ya Huduma inakuwa kwa kasi sana japo wao wanahudumia sana japo hawazalishi sana hivyo kwakuwa hapa ni kitovu cha watu wengi kufika hapa tutakuwa na mapato mengi sana kutokana na fursa zilizopo,"amesema.