Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:32 pm

NEWS: WATANZANI AFRIKA KUSINI WAANDAMANA KUTETEA MASHOGA

Pritoria: Watanzania waishio Afrika kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania nchini humo, wakipinga vikali kitendo cha serekali ya Mkoa wa Dar es salaam kupitia kwa mkuu wake Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa huo, hadi kimewafanya watu hao kushi kwa hofu kubwa.

Waandamanaji hao wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini.

“Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu. ilisema sehemu ya bango la mmoja ya waandamanaji


Tunakutaka uwape hifadhi watu hawa wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu” walisikika waandamanaji hao kwenye ujumbe wao.

Majuma ya hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini kitendo hiko kimekuwa kikipingwa na makundi mbali mbali ya haki za binadamu, wakisema ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.