Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:47 am

NEWS: WATANO MBARONI KWA KUGHUSHI NYARAKA NA KUIBA MILIONI 284

Pwani: Watu watano wakiwemo watumishi wanne wa serekali katika Hazina ndogo wilayani Kibaha wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali za malipo na kuiba Sh284.8milioni ambazo ni fedha za Serikali.

Taarifa zinasema kuwa Watuhumiwa wote wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Aprili na Mei, 2018, walishirikiana na ofisa mmoja wa Jeshi la Magereza mkoani humo.

Akizungumza leo Ijumaa Agosti 17, 2018 kamanda wa polisi mkoani Pwani, Jonathan Shanna amesema watuhumiwa hao waliiba fedha hizo kwa vielelezo zinazoonyesha zililipwa mzabuni wa kampuni ya Lukozi na Usambara Grocery and Vegetable Supplies ya mkoani humo. Shanna amewataja watuhumiwa hao Stanley Kansabala, (45), mkazi wa Kigamboni Dar es salaam, Boaz Lyimo (31), mkazi wa Kimara, Imani Kilembe (43), mkazi wa Suka ambaye yeye katika upekuzi anadaiwa kukutwa na Sh4.6milioni nyumbani kwake na Hallo Ntambi (38) aliyekutwa na Sh 4.2milioni nyumbani kwake, wote wakiwa ni wahasibu wa Hazina ndogo.

Mwingine ni ofisa wa Jeshi la Magereza mkoani hapa anayeshughulika na kazi za uhasibu SP Komango Makala (53) mkazi wa Magereza Kibaha na wote watafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapo kamilika.

Amesema pia wamemnasa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Lukola na Usambara, Omary Singano kwa mahojiano zaidi kwa kuwa kampuni hiyo ndiyo imeingiziwa fedha hizo, hivyo amemtaka kutii sheria bila shuruti kwa kufika ofisi ya mkuu wa upelelezi