- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WASIWASI WATANDA KUHUSU 'WANYONYAJI DAMU '.
MALAWI: Watu watano wameuawa kusini mwa Malawi baada ya kudaiwa kuwa na sifa na tabia za watu ambao huwanyonya wengine damu.
Umoja wa Mataifa umewaondoa wafanyakazi wake katika wilaya mbili kusini mwa nchi hiyo huku wasiwasi ukiendelea kuenea.
Taarifa zinasema marehemu waliuawa na makundi ya wakazi ambao waliwatuhumu kuwa walikuwa wanakunywa damu ya binadamu kama sehemu ya tambiko.
Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa na serikali kuzuia vifo zaidi.
Wakazi hawaruhusiwi kutoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri.
Umoja wa Mataifa umesema kwenye ripoti kwamba uvumi huo huenda ulianzia Msumbiji na kuvuka mpaka hadi kwenye wilaya za mpakani za Mulanje na Phalombe nchini Malawi.
Haijabainika wasiwasi umetokana na nini lakini kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo imenukuliwa na Reuters, wakazi waliweka vizuizi barabarani wakiwawinda "wanyonyaji damu".
Umoja wa Mataifa uliwaamuru wafanyakazi wake kuhamia maeneo salama kutokana na wasiwasi huo.
Rais wa Malawi Peter Mutharika ameapa kuanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo na afisi yake imetoa taarifa kwamba suala hilo "limeisikitisha serikali yote".
Mashirika mengi ya kutoa misaada hufanya kazi nchini Malawi, moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Viwango vya elimu ni vya chini mno na maeneo mengi huwa kuna imani za kishirikina.
Msururu mwingine wa mauaji kuhusu wanyonyaji ulikuwa umezuka huko mwaka