Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:05 pm

NEWS: WAPINZANI WAAZIMIA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA NCHINI KWAMUJIBU WA SHERIA

Zanzibar: Vyama vya upinzani nchini Tanzania ambavyo vimekuwa na mkutano wa kisisasa unaojulikana kwa jina Retret ulioitishwa na Katibu mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad visiwani Zanzibar vimeazimia kuanza kufanya mikutano ya hadhara kwa kuwa ni haki yao kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi.

Aidha Vyama hivyo vimetangaza rasmi kwamba wanasiasa wote waliopo jela kwa tuhuma za kisiasa hao ni ‘Wafungwa wa kisiasa’ na kuanzia sasa wataitangazia dunia hivyo.

Kama utakumbuka viongozo wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe yupo mahabusu kwa zaidi ya majuma kadhaa na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matico baada ya viongozi hao kufutiwa dhamana na mahakama ya Tanzania.

Tamko hilo limesainiwa na Maalim Seif, mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia; mwenyekiti wa NLD, Oscar Makaidi; naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu; mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Vyama hivyo vimetoa uamuzi huo wakati Serikali ya Tanzania ikiwa imepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya hadhara mpaka mwaka 2020 isipokuwa kwa wabunge walioshinda uchaguzi ambao wameruhusiwa kufanya mikutano kwenye majimbo yao tu.

Miongoni mwa viongozi wa upinzani walio mahabusu ni pamoja na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mhazini wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko ambaye pia ni mbunge wa Tarime Mjini.