- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAPINZANI CONGO WALALAMIKIA HITILAFU NYINGI ZA UCHAGUZI
Kambi kuu ya Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC imedai uchaguzi wa jana Jumapili ulikumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo kukwama kwa kompyuta za kupigia kura, na mvua kubwa katika maeneo mengi na vurugu kadhaa baadhi ya Maeneo.
Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Rais Joseph Kabila liliendelea hadi jioni katika baadhi ya vitongoji vya jiji la Kinshasa Jumapili, ambako vituo vilichelewa kufunguliwa kutokana na kukosekana kwa madaftari yenye orodha ya wapiga kura.
Mkutano wa maaskofu Katoliki wenye ushawishi DRC umesema mashine ya kupigia kura ambazo tangu mwanzo zililalamikiwa na upinzani zilikwama katika vituo 544 kati ya 12,300 walivyovikagua katika maeneo mbali mbali ya nchi.
Mmoja wa wagombea wanaopewa nafasi ya kushinda urais, Felix Tshisekedi amesema inaovyoonekana Kabila anaweza kuendelea kubaki madarakani, ikiwa uchaguzi utafutwa kutokana na hitilafu zilizobainika.
''Mambo yamevurugika kiasi kwamba tunashuku pengine ni vurugu za kupangwa, kwa makusudi ya kuipa Mahakama ya Katiba kisingizio cha kuufuta uchaguzi huu kesho.'' Amelalamika Tshisekedi.
Katika baadhi ya maeneo ya nchi, maafisa wa uchaguzi walianza kuhesabu kura kwa kutumia mwanga wa kurunzi, huku wakiziandika kwenye vibao vya madarasani. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa katika muda wa siku chache.
Ingawa kwa sehemu kubwa uchaguzi ulifanyika katika mazingira yenye utulivu kwenye maeneo mengi ya taifa hilo lenye eneo kubwa, kulikuwepo baadhi ya visa vya fujo.
Katika kituo kimoja cha kupigia kura katika jimbo la Kivu ya Kusini Mashariki mwa nchi, polisi alimpiga risasi na kumuuwa kijana mmoja baada ya kuzozana kuhusu madai ya ulaghai katika zoezi la upigaji kura.
Umati wa watu waliokuwepo walilipiza kisasi kwa kumpiga polisi huyo hadi kufa. Haya yamethibitishwa na mashahidi na wanasiasa waliokuwepo mahali hapo. Katika ghasia hizo, afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) pia aliuawa.