- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAWAKE WA UWT WAASWA KUCHANGUA VIONGOZI IMARA.
DODOMA: Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake(UWT)Mkoa wa Dodoma wameaswa kuchagua viongozi makini na imara watakaokifanya chama kiendelee kuwa imara kutokana na mkoa huo kuwa makao makuu ya Chama.
Rai hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dodoma alhaj ADAM KIMBISA wakati akifungua mkutano huo ambapo amesema CCM nyumbani kwake ni Dodoma hivyo viongozi watakaochaguliwa lazima watambue hilo kwa kulinda heshima isipotee.
Aidha amewaasa kutochagua viongozi wenye harufu ya rushwa bali wachague viongozi watakaokuwa wepesi wa kuwaunganisha akina na watakaoifanya jumuiya ijitegemee kiuchumi.
Amewaasa kupendana,kupungusa figisu,visasi,majungu,porojo bali wanyanyuane na kuinuana ili kila mmoja atomize yale aliyoyapanga kwa msaada mkubwa wa mwanamke mwenzake.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 473 ambapo miongoni mwa nafasi zinazogombewa ni nafasi ya uenyekiti UWT mkoa na wagombea wake ni Elizabeth Kazimila,Neema Majule na Lucy Rutahinurwa.
Nafani nyingine ni mjumbe wa baraza Kuu mkoa,mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa,uwakilishi kwenda wazazi mkoa,uwakilishi kwenda UVCCM mkoa na wajumbe wa baraza mkoa nafasi mbili kwa kila wilaya.