- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAWAKE NA VIJANA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA USHIRIKA
MLALO TANGA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) amewataka wanawake pamoja na vijana kuchangamkia fursa za uzalishaji uchumi zilizopo nchini kupitia vikundi vya ushirika.
Waziri Mhagama amesema hayo alipokutana na wakazi wa Kata ya Mwangoi iliyopo Jimbo la Mlalo, Wilaya ya Lushoto akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Tanga ambapo ameeleza kuwa, Serekali imejipanga kupiga vita umaskini, hivyo ni vyema wanawake na vijana wakaanzisha vikundi vya shughuli za kuhamasisha maendeleo.
Akizungumza katika hadhara hiyo, alisema Serikali ya awamu ya tano inatambua na imeendelea kuunga mkono juhudi za wanawake pamoja na vijana kupitia vikundi vya ushirika kwa lengo la kuboresha maisha ya kila mwananchi.
“Ninawahamasisha wanawake na vijana waone kipindi kilichopo sasa katika ukombozi wa kupambana na umasikini ni kujiunga kwenye vikundi vya ushirika, ili kuwa na nguvu ya pamoja itakayosaidia kuwajenga kiuchumi kwa kupata mikopo yenye riba nafuu na yenye tija kubwa” alisisitiza Mhagama.
Aidha Waziri Mhagama alieleza kuwa Sera ya vikoba, Serikali imeshaipitisha toka mwaka 2017 na hivyo kila Halmashauri zilishaagizwa zianze kusajili rasmi Vikoba kama taasisi zinazotambulika ili ziweze kukopesheka.
Aliongeza kwa kutoa maagizo kwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja na Mkurugenzi Ofisi ya Waziri, Idara ya Maendeleo ya Vijana kuandaa mafunzo maalum kwa vijana hamsini (50) kwenye sekta ya ufugaji nyuki, uhifadhi wa mazingira na utengenezaji wa asali. Ambapo vikundi hivyo vitapewa zana za kufanyia kazi ikiwemo mizinga na vifaa vingine. Kupitia mafunzo hayo vijana hao wataweza kufungua viwanda vidogo vidogo ikiwemo vya asali, vilevile wataweza kuvitumia vikundi hivyo kujipatia mikopo ambayo itawanufaisha kwa pamoja kama wanakikundi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Mhe. Rashid Shangazi alieleza kuwa vikundi hivyo vya ushirika vimekuwa viki hitaji fursa mbalimbali za kiuchumi lakini wamekuwa wakizikosa kutokana na kutokuwa na usajili rasmi ambapo imepelekea vikundi hivyo vya vijana na wanawake kushindwa kukopesheka.
“Tunayo Saccos yetu ya KUMEKUCHA MWAMKO ambayo inatumiwa kama Saccos ya mfano katika Mkoa wa Tanga, lakina bado haijanufaika na mikopo kutoka Serikalini kutokana na changamoto mbalimbali, na kuiomba Serikali kuwasidia kuanzisha benki ya jamii ambayo itavinufaisha vikundi hivyo vya ushirika na wakazi wa Mwangoi na Mlalo” alisema Shangazi.
Naye Katibu kikundi cha Mwamboa, Bw. Leonard Ngoda alisema kuwa kutokana na shughuli ambazo wamezianzisha kwenye vikundi kwa lengo la kujikwamua kiuchumi, lakini wameomba kupatiwa mafunzo endelevu ili waweze kuboresha ubora wa bidhaa ambazo wamekuwa wakizalisha hususan za kilimo, ufugaji nyuki na utunzaji mazingira.
“Endapo Serikali itatuwezesha kama vikundi kupata mafunzo pamoja ili litahamsisha kuendelea kujenga uwezo na kupiga hatua moja kubwa kimaendeleo“ alisema Ngoda.