- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAWAKE KENYA WAANZA KUWABEBEA WANAWAKE TASA UJAUZITO
Wanawake nchini Kenya wameanza kufanya kazi ya kubeba ujauzito kwa niaba ya wanamke waolewaji ambao ni tasa japo kwa masharti, katika juhudi za kutafuta ajira pamoja na kupambana na hali mbaya ya uchumi nchini humo.
Ni biashara ambayo haijakuwa na umaarufu hapa nchini lakini imekuwa ikiendelea kwa siri, japo kuna mikataba ya kisheria ambayo inafaa kuzingatiwa baina yake na familia ambayo haiwezi kupata mtoto.
Lakini viongozi wa dini wanapinga hali hiyo na kusema kuwa sasa jamii ina jinamizi ambalo watu kupata madhambi makubwa, huku wakionya waumini wa dini mbalimbali kufanya matendo mesma ambayo hayatomkasirisha Mungu.
“Ni jambo ambalo limeanza kuja sehemu za kwetu na ni jambo ambalo pia tunahitaji watu wajichunge, manake kuna wale ambao wanafanya hivyo kutunga mimba watoto wa kwenda kuuza, hilo hatuwezi kulikubali” amesema Martin Kivuva, askofu mkuu wa jimbo la Mombasa.
Gunga Mwinga. Mwanasheria nchini Kenya, anasema suala hili bado ni nyeti nchini humo kutokana na maadili ya jamii, japo kunafaa kuwa na mkataba wa kisheria baina ya pande zote mbili.
“Ni swala ambalo ni jipya, halijaweza kuingia sana katika akili za binadamu hasa katika Jamuhuri yetu ya Kenya,” amesema Bw Mwinga
Hata hivyo raia nchi Kenya ambao waliweza kuongea na Idhaa ya Kiswajili ya RFI wanasema swala hili haliambatani na maadili ya jamii na ni la kupotosha.