Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:34 pm

NEWS: WANAWAKE 2 WATANDIKWA VIBOKO HADHARI KWA KUFANYA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Nchini Malaysia wanawake wawili waliokutwa na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja ndani wamechapwa viboko hadharani kwenye mahakama ya kidini.

Wanawake hao wafuasi wa dini ya kiislamu mmoja anaumri wa miaka 22 na mwingine 32 kila mmoja alichapwa viboko sita kwenye mahakana ya Sharia katika jimbo la Terengganu.

An Acehnese woman is lashed by a hooded local government officer during a public caning at a square in Aceh province, on June 12, 2015.

Kulingana na afisa mmoja ni kuwa hiyo ndiyo hukumu ya kwanza inayohusu mapenzi ya jinsia moja na ndiyo adhabu ya kwanza ya kuchapwa hadharani.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali hatua hiyo ya kuchapwa kwa wanawake. Kuchapwa huko kulishuhudiwa na zaidi ya watu 100 kwa mujibu wa vyombo vya habari.

Mwanachama mmoja wa baraza kuu la Terenggau, Satiful Bahri Mamat, alitea adhabu hiyo, akiliambia shirika la Reuters kuwa hatua haikuwa na ya kutesa au kuumiza, na ilifanyika hadhari ili iwe funzo kwa jamii.

Wawili wao ambao majina yao hayakutajwa walimamatwa mwezi Aprili na maafisa wa kulinda itikadi za kiislamu baada ya kupatikana ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa eneo la umma huko Terengganu.

Wote walikiri kuvunja sheria za kiislamu na walihukumiwa kuchapwa viboko na faini ya dola 800.

"Vitendo vya kingono kati ya watu wawili wazima havistahili kuchukuliwa kama uhalifu, au kuadhibiwa kwa viboko," shirika linalowahudumia wanawake lilisema.

Kulingana na shirika hilo, kuchapa viboko chini ya sheria za kiislamu haifanani na adhabu ya viboko inayofanywa kwa uhalifu mwingine chini ya sheria za kiraia. Haina lengo la kuzua machungu.