November 29, 2024, 6:30 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAUME KUPIGWA VIBOKO 12 WATAKAO SIMAMA NA MWANAFUNZI WA KIKE
GEITA; Uongozi wa kata ya Nyehunge wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwapiga viboko 12 au faini ya Sh10,000 wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, Wilaya ya Tandahimba imekamata wanafunzi watano waliopata ujauzito mwaka jana.
Sheria hiyo ndogo imepitishwa juzi kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WODC) baada ya tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata uja uzito kuzidi kuwa sugu.Ofisa mtendaji wa Kata ya Nyehunge, Mabula Enock alisema sheria hiyo itasaidia kudhibiti vitendo vya wanaume wanaoshawishi wasichana kufanya nao mapenzi na baadaye kuwapa ujauzito unaokatisha ndoto zao.“Tumelazimika kupitisha sheria hiyo ili kuungana na mkuu wa wilaya yetu, Emmanuel Kipole aliyeagiza wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wacharazwe viboko au kutozwa faini ya Sh10, 000 ama vyote kwa pamoja,” alisema Enock.Agizo la mkuu huyo wa wilaya alilitoa Oktoba mwaka 2017 wakati akikaribisha wanafunzi 81 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Nyehunge.
Newest Posts