Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:52 pm

NEWS : WANAOVURUGA UHUSIANO NA IRAN NA AZERBAIJAN KUCHUKULIWA HATUA

Kiongozi: Hatua zichukuliwe dhidi ya wanaovuruga uhusiano wa Iran na Jamhuri ya Azerbaijan

  • Kiongozi: Hatua zichukuliwe dhidi ya wanaovuruga uhusiano wa Iran na Jamhuri ya Azerbaijan

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa kuna wanaopinga uhusiano wa karibu na wa udugu baina ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan, na kwa msingi huo kuna ulazima wa kukabiliana na wanaotekeleza njama hizo.

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo Jumatano alasiri mjini Tehran wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Ilham Aliyev, Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan ambapo aliashiria mshikamano wa kina baina ya nchi mbili na ulazima wa kuimarisha ushirikiano. Amesema Tehran na Baku zina motisha maradufu wa kuimarisha uhusiano katika sekta mbali mbali.

Ayatullah Khamenei ameashiria ukweli kwamba, aghalabu ya watu wa Jamhuri ya Azerbaijan sawa na watu wa Iran na Iraq ni wafuasi wa madhehebu ya Ahul Bayt AS na kuongeza kuwa: "Tunapaswa kuthamini fursa hii hasa hafla za maombolezo ya Ashura miongoni mwa Mashia wa Jamhuri ya Azerbaijan ambayo yanaimarisha zaidi utambulisho wa taifa na nchi hiyo.

Rais Ilham Aliyev wa Jamhuri ya Azerbaijan na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema sababu ya kufeli Shirikisho la Sovieti lilikuwa ni kuhimiza Umaxi na upuuzaji dini miongoni mwa watu wa Azerbaijan. Amesema pamoja na hayo imani ya watu wa Jamhuri ya Azerbaijan iliimarika na mfano wa hilo ni kufanyika kwa ufanisi maombolezo ya Muharram mwaka huu.

Kwa upande wake, Ilham Aliyev amesema anaitazama Iran kama nyumba yake huku akiashiria kuzidi kuimarika uhusiano wa nchi mbili. Amesema Jamhuri ya Azerbaijan ina uhusiano imara kabisa na Iran na kwamba nchi yake haitamruhusu mtu yeyote avurige uhusiano wa pande mbili. Aliyev amesema Jamhuri ya Azerbaijan inataka kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kiutamaduni na Iran.