Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:05 pm

NEWS: WANANCHI WAPANGA KUMBURUZA DC MAHAKAMANI

Kilimanjaro: Wananchi wa Kijiji cha Chekereni Weruweru kata ya Kindi mkoani Kilimanjaro wamepanga kumfikisha Mahakamani Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba, kwa tuhuma ya kuvamia na kuvunja Ofisi ya kijiji hicho na kuchukua nyaraka muhimu za ofisi hiyo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, John Bosco, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Desemba 19, 2018 kijijini hapo.

“Tunataka mahakama itafsiri kuwa ofisi ya Kijiji cha Chekereni Weruweru ni mali ya Serikaliya kijiji au CCM… mkuu wa wilaya ametumia vigezo gani kuhalalisha kuwailikuwa mali ya chama hicho na kudiriki kuja kuvunja ofisi yetu. Tulitegemea yeye ndio atatue migogoro,lakini amekuwa sehemu ya kuichochea,” alisema.

Bosco alisema kiongozi huyo amekuwa ni sehemu ya kuchochea migogoro na kwamba hawapotayari kuchonganishwa bali watafuata sheria.

Alisema mgogoro huo ulianza baada ya mkuu huyo wa wilaya, kutumia nguvu nakuwanyang’anya kijiji ofisi yake na kukipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo ndio chanzo cha mgogoro huo.

Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho, Omari Omari, alisema ofisi hiyo walikabidhiwa Februari 2, 2015 na Serikali ya kijiji iliyotangulia baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014.

“Ofisihii ni mali ya kijiji, tulikabidhiwa jengo, nyaraka na eneo la kijiji hekta 42,175, hakuna mahali imeandikwa hii ni ofisi ya CCM, tumeitumia kwa miaka yotetangu izinduliwe mwaka 1993 na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Agustino LyatongaMrema,” alisema.