Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:24 am

NEWS: WANANCHI WAMPA WAZIRI MKUU MAJINA YA MATRAFIKI WALA RUSHWA

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amepewe majina na Wakazi wa Tanga ya Matrafiki ambao ni vinara kwa kuomba rushwa kwa madereva wa Noah wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Naye Majaliwa akamkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela orodha ya matrafiki hao.

Majina ya trafiki hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa madereva wa noah wanaofanya kazi ya kusafirisha abiria ndani ya wilaya hiyo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu kupitia mabango.

Waziri Mkuu alimkabidhi Mkuu wa Mkoa majina hayo jana jioni (Jumatano, Oktoba 31, 2018) baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sabasaba, Lushoto mjini.

Baada ya kumkabidhi majina hayo alimuagiza afanye uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili askari hao na kisha awasilishe taarifa kwake leo Alhamisi Novemba 1, 2018.

Mbali ya wananchi kuwasilisha malalamiko hayo, Pia mbunge wa Lushoto, Shaaban Shekilindi alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kutatua kero hiyo inayowakabili wananchi.

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Lushoto katika ukumbi wa chuo cha Mahakama Lushoto ambapo aliwasisitiza wafanye kazi kwa bidii.